RUVU SHOOTING WAONA MAMBO MAGUMU...WAMPIGIA MAGOTI EMMANUEL OKWI NA KUFUNGUKA HAYA

Uongozi wa klabu ya Ruvu Shooting inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara umeomba radhi kufuatia tukio lisilo la kiungwana la mchezaji wake Mau Bofu kumpiga kiwiko mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi.

Bofu alifanya tukio hilo katika dakika ya 43 ya mchezo uliozikutanisha timu hizo Jumapili iliyopita katika Uwanja wa Uhuru na kurushwa mbashara kupitia Azam Sports 2, na kusababisha Okwi asiweze kuendelea na mchezo na yeye kutolewa nje kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja.

Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema wao kama uongozi pamoja na mchezaji mwenyewe wamekiri kufanya kosa hilo na wanamuomba radhi Okwi mwenyewe, uongozi wa Simba pamoja na wapenda soka wote.

No comments: