HAJI MANARA ACHACHAMAA KWA ALIYEMPIGA OKWI,AFUNGUKA MAZITO

Haji Manara acharuka kwa Aliyempiga Okwi,Azungumza Haya

Afisa Habari wa Timu ya Simba Haji Sunday Manara amesema Kuwa mchezaji aliyempia Emmanuel Okwi asiishie kupewa adhabu ndogo na Badala yake apewe adhabu Kubwa

” Nitoe wito kwa TFF na Timu nyingine Tunaweza kupoteza uhai wa mchezaji kwa makosa ya Kipuuzi puuzi ,Adhabu za makosa kama yale ziwe kubwa sana zisiishie tu mechi 3 au mechi 2 hapana unampiga Mtu sehemu mbaya chochote kinaweza kutokea, Mpira wa Miguu ni mchezo wa Kiungwana. “

Mchezaji Mau Bofu ndiye aliyempiga Okwi maeneo ya Koromeo hali iliyomfanya Okwi kushindwa kuendelea na Mchezo kati ya Simba na Ruvu Shooting.

Haji Manara pia Kuelekea mchezo Dhidi ya Azam Fc wamejipanga vyema huku wakiingia Dimbani wakiwa wanawaheshimu Azam Fc kutokana na kuwa na Timu nzuri yenye kikosi kipana lakini nao pia wanaamini kwenye Kikosi chao.

Huku akiwaomba Mashabiki wa Simba Kuhudhuria kwa Wingi kesho kuishangilia Simba.

No comments: