Mkubwa ni mkubwa tu:KOCHA MKUU WA SIMBA ATANGAZA KIAMA.... AWAPA NENO ZITO WACHEZAJI WAKE
Baada ya Simba kuitumbua Azam FC, Kocha Mkuu wa Simba, Pierre Lechantre amewataka wachezaji wake kuhakikisha wanadumisha mwendo wao walionao kwa sasa.
Lechantre amezungumza na wachezaji wake na kuwapongeza namna wanavyokenda kutokana na hali ilivyo katika Ligi Kuu Bara.
“Kocha amewapongeza wachezaji kwa mwendo mzuri wanaokwenda nao katika ligi.
“Lakini amewasisitiza kuwa makini kwamba ligi haijaisha na bado hawajabeba ubingwa. Hivyo wanatakiwa kuendelea kujituma na kudumisha nidhamu ndani na nje ya mchezo,” kilieleza chanzo.
Simba sasa inaongoza Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 41 na itakuwa na mapumziko ya ligi ikienda katika michuano ya kimataifa.
Mfaransa huyo anasaidiwa na makocha watatu ambao ni Masoud Djuma raia wa Burundi, Mohamed Habibi kutoka Tunisia na Mwarami Mohamed ambaye ni Mtanzania.
No comments: