Breaking News: HABARI MPYA KUTOKA KLABU YA YANGA ZILIZOTUFIKIA HIVI PUNDE

Yanga wameanza leo maandaliii ya mwisho ili kuwavaa Mabingwa wa Shelisheli, St Louis kwa kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Polisi jijini Dar es Salaam, leo.

Yanga inafanya mazoezi leo asubuhi kwenye Uwanja wa Polisi huku baadhi ya wachezaji ambao ni majeruhi wakitarajia kurejea.

Mechi hiyo ya Ligi ya Mabingwa Afrika itapigwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na tayari St Louis wako nchini.

Tayari St Louis nao wameanza kujiandaa na mechi hiyo kwa kufanya mazoezi jijini Dar es Salaam.

Mabingwa hao wa Shelisheli wanaamini kufika mapema nchini ni kupata nafasi ya kuzoea vizuri mazingira na hali ya hewa ya Tanzania.

No comments: