HIZI HAPA SABABU KWANINI WANAWAKE WENGI HAWAPENDI KUTOKA NA WANAUME WAFUPI
Kuna utafiti niliusoma siku moja kuhusu wanaume wafupi, na walisema wanaume wafupi wana mapenzi ya kweli na ya dhati kuliko wanaume warefu, kitu ambacho siwezi bisha sababu, wanawake wengi huwa hawapendi kutoka na wanaume wafupi kwahiyo inawachukua sana muda kupata mwenza na lazima wawapende na wawape mapenzi ya kweli wanawake zao ili wasiwaache kwa sababu wanawake wengi wanapenda mwanaume warefu na wengi wana mvuto kuliko wafupi.
Wanawake wengi wanapenda kutoka na wanaume ambao wamewazidi urefu hata kidogo, kuliko kuwa na mwanaume ambaye ni mfupi kuliko wao,wengi wanasema hii inaleta picha mbaya au muonekano mbaya wakiwa wanaongozana wanaita (not Marching), lakini kuna sifa nyingine za wanaume wafupi wanawake wengi wanasema zinawakera kama,
Wivu
Inasemekana wanaume wafupi wana wivu wa kupindukia na sio kama wanaume wengine warefu hawana wivu ila wao wivu wao unapitiliza kiasi cha kukera kwani wivu ukizidi sana ni kero katika mapenzi.
Sifa
Wanaume wengi wafupi wana sifa sana, kiasi cha kukera wanajisifia sana, na wanataka sana kuonekana, kama wapo eneo Fulani wakiingia sehemu mtajua kama kuna mtu kaingia sababu ya sifa zao na maneno yao japokuwa pia wana sifa moja ya kuwa wachechi sana.
Gubu
Hapa sasa ukichanganya na wivu ni balaaa maana mwanaume mwenye gubu ni zaidi ya mwanamke muongeaji, Gubu ni ile hali ya kukosoa kila kitu,kila kitu kibaya, yeye haridhiki na chochote na hata utaonekana huwezi chochote akiwa karibu, hilo gubu au hata kama kila kitu kipo sawa atatafuta sababu ya kuongea tu.
Wanajidai Wanajua kila kitu. ( Much know)
Much knows, hapa bwana unakutana na mtu kila kitu anajua yeye, ni kero sababu akiwa mbele za watu atataka kila mtu ajue anajua nini kama inaongelewa siasa, mpira au mapenzi yeye fundi wa kila kitu, kitu ambacho kiukweli kinakera sana wakati mwingine.
Muonekano/ Mvuto
Wanawake wengi wasema wanaume wafupi hawana mvuto sana, kama wanaume warefu, kwahiyo hiyo ni moja ya sababu ya wao kutotaka kutoka na wanaume wafupi, japokuwa sio wanaume wote wafupi hawana mvuto. Japokuwa inasemekana siku hizi hakuna anaeangalia urefu wako uzuri wako watu wanangalia sana mfuko wako tu, hayo ni maneno ya mitaani watu wanaongea. Mimi binafsi sijui kama ni hali halisi.
No comments: