HABARI NJEMA KUTOKA KLABU YA YANGA USIKU HUU...NI BAADA YA KUIGARAGAZA NJOMBE MJI MABAO 4-0
Emmanuel Martin ameonyesha ukomavu kwenye mchezo wa leo kwa kutengeneza bao la mwisho, huku Yanga ikiibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Njombe Mji mchezo ulipigwa kwewnye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo jumanne.
Mabao ya Yanga yalifungwa na Obrey Chirwa aliyetupia wavuni matatu (46', 65 na 87) huku la Emmanuel Martin akiweka moja dakika ya 69.
Chirwa sasa amefikisha mabao 10 akiachwa magoli mawili na Emmanuel Okwi anayeongoza akiwa na mabao 12 huku akimpita John Bocco mwenye mabao 9.
Maeneo ambayo Yanga imeyatumia zaidi ni eneo la upande wa kushoto na eneo lake la kati (kiungo) upande wa kulia ambao anacheza Raphael Daud na Hassan Kessy wanaonekana kucheza kwa kufanya majuku mengine na sio kushambulia.
Ushindi wa leo unaifanya Yanga kufikisha pointi 34 na kusogea nafasi ya pili ikiisogelea Simba yenye pointi 38.
No comments: