HABARI NJEMA KUTOKA KLABU YA SIMBA ZILIZOTUFIKIA HIVI PUNDE,ZINAMHUSU MFUNGAJI WA JANA EMMANUEL OKWI
Mshambuliaji huyo raia wa Uganda amefikisha jumla ya mabao 13 kwenye ligi, jambo zuri au la kushangaza kuhusu Okwi ni kwamba magoli yake yote ameyafunga kwenye viwanja vya Dar (Uwanja wa Uhuru na Uwanja wa taifa).
Amefunga magoli nane (8) kwenye uwanja wa Uhuru huku magoli matano akifungia uwanja wa taifa. Hajafunga goli hata moja kwenye viwanja vya nje ya Dar katika mechi ambazo amecheza mikoani.
Mechi ambazo Okwi amefunga hadi sasa kwenye ligi kuu Tanzania bara
Simba 7-0 Ruvu Shooting (Okwi alifunga magoli manne, akawa mchezaji wa kwanza kufunga hat-trick msimu huu -Uwanja wa Uhuru.)
Simba 3-0 Mwadui (alifunga magoli mawili na kufikisha magoli sita -Uwanja wa Uhuru)
Simba 1-1 Mtibwa Sugar (akaendeleza rekodi ya kufunga mfululizo kwenye uwanja wa Uhuru na kufikisha magoli saba yote akiyafunga uwanja huohuo -Uwanja wa Uhuru.)
Simba 4-0 Njombe Mji (Okwi alifunga goli (1) la kwanza katika mchezo huo-Uwanja wa Uhuru)
Simba 4-0 Singida United (Okwi alifunga magoli mawili-Uwanja wa taifa)
Simba 4-0 Majimaji (Okwi alifunga magoli mawili-Uwanja wa taifa)
Simba 1-0 Azam (Okwi amefunga bao pekee katika mchezo huo-Uwanja wa taifa)
No comments: