BAADA YA SIMBA KUIGARAGAZA AZAM,HAJI MANARA ATUMA BONGE LA UTANI KWA YANGA

Wekundu wa Msimbazi Simba SC Jumatano ya February 7 2018 walikuwa uwanja wa Taifa DSM kucheza mchezo wa marudiano wa Ligi Kuu dhidi ya Azam FC, Simba katika game hiyo walifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0 limefungwa na Emmanuel Okwi dakika ya 37.

Goli hilo la Okwi linakuwa ni goli lake la 13 katika Ligi msimu huu akiongoza katika list ya wafungaji hadi sasa, baada ya game hiyo afisa habari wa Simba Haji Manara ametumia ukurasa wake wa instagram kuhoji kuhusiana na wale waliokuwa wanambeza Okwi na kumtania kuwa mhenga.

“Hivi kale kamsemo kuwa Okwi ni mhenga bado kapo huko kwenu? Au kale kamsemo kuwa naniliu kashushwa na Mungu sikisikii siku hz, Muweke akiba bandugu,,mpo kimyaaaa kama mwanga alioanguka na Ungo sokoni…Bumbaaaaav  @emmanuelokwi @nyoni #gongowazi#gongowazi

No comments: