NJIA NZURI ZA UZAZI WA MPANGO

uzazi wa mpango sio kitu kibaya, wataalamu waligundua njia hizi ili kupunguza idadi kubwa ya watu hasa kwenye ngazi ya familia ambapo kuwahudumia inakua kazi sana...kwa dunia ya sasa hivi kuzaa watoto kwanzia watano kwenda mbele basi kuwasomesha na kuwatunza sio kazi rahisi.
zipo njia ambazo hazitumii dawa au kemikali zozote kwa mfano kondomu, kuchomoa uume kabla ya kufika kileleni, kalenda na kunyonyesha mtoto..hizi hazina madhara kabisa kwenye mwili wa binadamu lakini zipo zinazotumia kemikali ambazo zipo kwenye mfumo wa homoni kama za binadamu yaani oestrogen and progesteron.

homoni hizi zinapatikana kwenye mwili wa binadamu kama homoni za uzazi lakini kuna jinsi unaweza kuzitengeneza maabara ukampa mwanamke ili asipate mimba.
kwa hali ya kawaida ili upate mimba basi homoni hizi lazima ziwe kwenye kiwango maalumu..kupungua mwilini au kuongezeka mwilini kwa kiwango hichi cha homoni kunazuia mimba kabisa.

dawa hizi zinafanyaje kazi?
hufanya kazi kwa kuzuia yai la mwanaume kufika mwenye mfuko wa uzazi wa mwanamke, huzuia yai kutengenezwa kutoka kwenye kiwanda cha mayai cha mwanamke[ovari], huzuia yai kushuka kutoka kwenye ovari kwenda kukutana na mbegu ya mwanaume. mfano wa dawa hizi ni zile za kumeza kila siku, kitanzi, sindano ya kila miezi mitatu na vijiti.
nini madhara ya kutumia njia hizi?
kuna madhara madogo madogo kama kichefuchefu, kutapika, kizunguzungu, matiti kuuma na kadhalika lakini kuna yale madhara makubwa ambayo ntaenda kuzungumzia leo.
kuongezeka uzito au kunenepa; wanawake wengi wanaotumia dawa hizi ni wanene sana kuliko wale wasio tumia, tafiti zimeonyesha dawa hizi zinaongeza sana hamu ya kula na kumfanya mtumiaji ale sana kuliko kiwango cha kawaida lakini pia huzuia kiwango cha maji ya mwili kutoka nje kwa njia ya mkojo.
kuchelewa kupata uzazi; baadhi ya dawa za uzazi wa mpango huchelewesha sana mtu kubeba mimba baada ya kuziacha, mtu huweza kukaa mpaka miaka mitatu bila kubeba mimba wakati tayari ameshaacha dawa.mfano sindano
kupotea kwa hamu ya tendo la ndoa; kwasababu dawa hizi zinaenda kuvuruga mfumo wa kawaida wa homoni za mama, ambapo mfumo huo huo ndio unahusika kumpa mama hamu ya tendo la ndoa basi wanawake wengi hujikuta hawajisikii kushiriki kabisa tendo hili.

saratani ya kizazi; tafiti mpya zimeonyesha kuna mahusiano makubwa sana kati saratani ya kizazi na matumizi ya dawa hizi, wagonjwa wengi wa saratani ya kizazi walikua na historia ya kutumia dawa hizi.

chunusi; dawa za uzazi wa mpango ni msumeno unaokata mara mbili, wapo ambao wakitumia chunusi zote zinaisha kabisa na wapo ambao wakizitumia chunusi ndio zinaongezeka zaidi na hii yote ni sababu ya mabadiliko ya homoni.

saratani ya matiti; mabadiliko haya ya viwango vya homoni yanasababisha saratani ya matiti kwa watumiaji wengi wa dawa hizi japokua sio wote wataugua lakini inamuweka mtumiaji kwenye hatari hiyo.

presha, kiharusi na ugonjwa wa moyo; dawa za uzazi wa mpango zinagandisha damu ya mtumiaji, kuganda huku kunasababisha kuziba kwa baadhi ya mishipa ya damu hii huleta magonjwa ya moyo na presha.
mabadiliko ya maji maji ya uke; baadhi ya watu hujikuta wakitoa maji mengi sana kwenye uke wakati wa tendo la ndoa na wengine huweza kukaukiwa na maji hayo.
hasira; watumiaji wa dawa hizi wakati mwingine hua na mabadiliko ya maelewano na watu au mood, yaani mtu anaweza kuacha kuongea na wewe ghafla bila sababu yeyote au akapata haisira za ghafla wakati ulikua unaongea naye hapo nyuma.

maumivu ya kichwa na kushindwa kuona vizuri; baadhi ya watumiaji hujikuta wanapata maumivu makali ya kichwa na ya muda mrefu lakini pia dawa hizi huzuia maji ya mwili kutoka nje na kuongeza presha ya macho hii humfanya mtumiaji ashindwe kuona vizuri.

kukatika kwa nywele; dawa hizi zinasababisha nywele kukatika kwa baadhi ya watumiaji lakini sababu yake haifahamiki vizuri.

mwisho; makala hii hailengi kuwaambia watu waache kutumia dawa hizi, lengo ni kuwaonyesha madhara yake ili wazitumie huku wanajua au wahamie kwenye njia zingine salama zaidi, kwa waathirika wa madhara ya dawa hizi unaweza ukapata matibabu kulingana na tatizo ambalo limekupata baada ya kuzitumia...unaweza kututafuta kupata matibabu hayo.

No comments: