MAMBO 15 AMBAYO WANAUME WANAYATAKA KATIKA MAHUSIANO (LAKINI WANAWEZA WASIKUAMBIE)
Hatutapiga kelele,au kuandika, au kuweka na kuonyesha katika profile,au kuongelea hilo sisi wenyewe.
Hapana. Wanaume wengi hawana tabia ya kusema wanachohitaji, lakini naweza kukuambia kutokana na uzoefu wangu mwenyewe, ingawa sio yote, wanaume wanakutaka na kukuhitaji uwafanyie vitu kama vifuatavyo.
1.WEMA WAKO.
Ulimwengu unaweza ukawa na ukatili na uonezi na adhabu ,kazi zetu zinaweza kuwa mbaya, na kukawa na ushindani mwingi, tunashughulika na kuhukumiana na kutofautiana kwa wale walio karibu yetu, kuhukumiana kidogo, kusameheana kidogo na uelewa kutoka kwa wanawake tunaowapenda umeenda mbali.
2.FURAHA YAKO.
Tuambie umefurahi, tuonyeshe furaha, tunahitaji kuwepo karibu yako unapokuwa na furaha, tutakuwepo wakati ukiwa na hali mbaya, kwenye tatizo lolote, lakini furaha yako ndio itakayokuwa inatuvuta kuwepo karibu na wewe, pamoja na kwamba yanatuhusu sisi hayo.
3.SIFA NA SHUKRANI ZAKO.
Muda mwingine tunafanya vitu vizuri, tuambie kuwa unashukuru na unathamini hicho na jinsi ulivyopendezwa na na hicho na kukufanya uwe mwenye furaha, Onyesha kuwa umeshukuru kuwa na wao katika maisha yako, na unakubali company yao, mchango wao, na ushirikiano.
4.IDHINI YAKO.
Hatupendi kukubali, lakini mara nyingi huwa hatufikirii kuwa kibali chako ndicho tunachohitaji, jinsi tunavyoishi au kutenda.Chukua hio nafasi wakati tunapokuwa sahihi kuturuhusu kufahamu kwamba umekubali.Tuambie umekubali maamuzi yetu, uchaguzi wetu,au jinsi tunavyoshughulikia vitu, tuambie unafurahishwa na sisi na unaona fahari kuwa na sisi.
5.MGUSO WAKO.
Tunahisi mguso wako , kujali kwako, mabusu yako, urafiki wako kwetu ni muhimu sana-yawezekana ni kidogo lakini ni muhimu .unapotugusa tunahisi kupendwa, unapokuwa muwazi kwetu kwa upendo mwingi,unatufanya tujisikie ulimwengu ni wetu wote.
6.SHAUKU YAKO.
Tunakutaka wewe ututake sisi, tuambie kwamba uko ndani, jielezee shauku yako kwetu.
7.NGUVU YAKO NA KUSAIDIA.
Tunakuhitaji sana pale tunapopita katika changamoto nyingi za maisha yetu. Hata kama hatuwezi kuongelea hicho, tunahitaji mtu mwenye nguvu ya kimya kimya, tunahitaji mtu wa kutuweka sawa, kusaidia,na kututia moyo, tuambie tuko nyuma yako tunapokuwa tunapita katika matatizo mbalimbali.tunaweza tusiongelee hilo , lakini uwepo wako pale tunapokuhitaji ni muhimu kwetu.
8.UELEWA NA UWEPO WAKO.
Sisi ni watatuzi na tunapenda kutatua mambo.tunaposhughulikia matatizo, hatuhitaji ufumbuzi zaidi ya kukuhitaji uelewa wako na uwepo wako.inaweza kuwa hatuongei ni kitu gani kinatutatiza, lakini ukiwepo, na kuelewa na kuwa msaada hicho ndicho tunachotaka. Tunachotaka ni kujua kuwa hatupo peke yetu.
9.UNYENYEKEVU WAKO NA UWEZO WA KURUHUSU.
Tunataka mwanamke mwenye kutuheshimu na anaeleta usawa, tunataka mwanamke anaekubali kufikia mwafaka na ambaye anakubali kwa upesi bila kinyongo tunapoharibu.hashikili neno, anaweza kuachia bila kinyongo na kutoa nafasi tena.
10.UKWELI WAKO.
Kama wewe, tunahitaji tujisikie kuwa sisi ni pekee katika maisha yako. Tusaidie tujisikie tunahitajika zaidi kwako kwa kutuonyesha kwamba una wajibu kwetu. Uwepo pale tunapokuhitaji, tusaidie kuliko mtu mwingine yeyote.
11.UAMINIFU WAKO.
Tunathamini uaminifu wako na kutuamini sisi, tunakutaka uwepo na sisi pale tunapokuhitaji , na kutuonyesha kuwa unajali.Kwa inshara hio hio tunataka uamini kwamba tunategemewa, tunawajibika,na tutakuwa pale unapohitaji tuwepo.
12.UVUMILIVU WAKO.
Sisi sio wakamilifu,inawezekana sio mwanaume ambae ulimtarajia, tunakubali uvumilivu wako kwa kutusaidia kukua katika mtazamo tunaoweza kuwa,hatuwezi kubadilika mara moja . msisitizo wako na uvumilivu wako utatufanya kubadilika jinsi unavyotaka tuwe.
13.MOYO MSIKIVU NA UCHESHI.
Maisha ni ya muhimu na ya kuchukulia umakini sana, watu hufanya makosa, hujikwaa,na hata kumsikitisha mtu, tunapopita katika magumu, mambo yanapotuchanganya ulimwenguni, tunahitaji kuwa na mtu fulani ambae atakupa furaha katika mambo madogo, ucheshi wako,furaha yako na kuonyesha kujali hutufanya tufurahie maisha zaidi.
14.URAFIKI WAKO.
Tunahitaji urafiki wako kila siku na kila mara.tunataka kufurahia muda na wewe, tunahitaji kushiriki mvuto wako, kutengeneza urafiki na kuteka mioyo yetu.
15.UMBALI WAKO (WAKATI MWINGINE).
Sio kwamba sisi ni wanaume wanaopenda kuishi kwenye mapango, wale wanaohitaji muda mwingi kuwa peke yao kama tunavyotaka kufanya kwako, Lakini tunahitaji kupata muda kidogo tu ili kucharge hisia wakati mwingine, zawadi kubwa ambayo tunataka kutoka kwako ni kutoa muda ili tuwepo peke yetu ili kujiona kuwa tunakuhitaji. Inatupa balance na nafasi ya kukuhitaji zaidi.
Jipange .
mimi nimeanza kuelewa , kuvuliana , kuamini,kuwa mkweli , kuwa mnyenyekevu n.k . je wewe?
No comments: