SABABU ZA WATU KUFUMBA MACHO WAKATI WA KUBUSU

Ulishawahi kujiuliza kwanini watu wengi waliopo kwenye mahusiano ya kimapenzi hufumba macho yao wakati wa kubusu? Hakuna sheria iliyopitishwa kuwataka wafumbe macho lakini hufumba, na kwanini unatakiwa ufumbe macho? Twende pamoja katika makala hii kuelewa sababu chache.

1. Acha midomo yako iongee

Kabla ya wapenzi hawajaanza ku kiss, huwa na muda wa kuzungumza na kujadiliana mambo kadha wa kadha yanayohusu maisha yao. Sasa inapofika wakati wa kubusu, ni muda wa kuacha midomo (lips) zako zielezee ile habari ambayo usingeweza kuisema. Hivyo watu hufumba macho ili kuacha midomo yake pekee ndiyo iwe inafanyakazi wakato huo.

2. Ni ishara ya raha

Kwa kawaida, binadamu hufumba macho yake pale anapofanya au kusikiliza kitu kinachouburusisha moyo wake na kufanya awe na furaha. Fikiri wakati unasikiliza mziki mzuri, ukila kitu kitamu, ukiimba kwa hisia, ukifika kilele. Hivyo kufumba macho wakati wa kubusu, ni njia ya kuonyesha kuwa unaburudika.

3. Ni ishara ya uaminifu

Mtu akiwa amesimama sehemu ya hatari au kujiegemeza, huwezi ukamwambia afumbe macho akakuelewa kwa sababu si sehemu salama lolote linaweza kutokea. Lakini wakati ukiwa unabusu na mpenzi wako, upo sehemu salama isiyo na hatari, huhitaji kufumbua macho uangali nini kinakuja kwa sababu unauhakika upo sehemu salama.

4. Huongeza kufurahia

Unapofumba macho na kuyaelekeza mawazo yako kwenye kile unachokifanya, inakufanya uwe na hisia zaidi, mawazo yako yawe kwenye kile unachokifanya, na hivyo kukufanya usikie raha zaidi.

5. Huonyesha hali ya kujisalimisha

Hii ni ishara kuwa umejisalimisha kwa huyo uliyenaye, haufanya mambo kwa haraka na kukurupuka. Ni sawa na kumkabidhi mtu mwili wako na hisia zako.

6. Kuepuka vitu vya ajabu

Kwanza baadhi ya watu huogopa kuangaliana kwenye macho, hivyo ili kuondoa ile aibu wakati anakubusu,inamlazimu kufumba macho awe kama amejitoa ufahamu. Pili, kuepuka vitu vinavyoweza kukutoa uweponi nwa unachokifanya. ‘Attention’ ni jambo la muhimu kufurahia unachofanya.

7. Kujiweka sawa (turn on)

Watu hufumba macho ili kujitenga na yaliyokaribu nao au kwenye akili zao. Katika lugha ya kimapenzi unaweza kusema anajipeleka ulimwengu mwingine wa mahaba. Anajiweka mwili wake kuwa tayari kwa ajili ya mambo yanayofuata.

No comments: