JINSI YA KUMFANYA MWANAMKE AMSAHAU MPENZI WAKE WA ZAMANI
Naamini hii hali ishawahi kukutokea wakati mmoja au mwengine, kuna mwanaume flani ambaye umependezwa naye lakini bado fikra zake ameziweka kwa mpenzi wake wa zamani. Ama umeanza kuchumbiana na mwanaume halafu baadae ukagundua kuwa huyu mwanaume mara kwa mara anamtaja mpenzi wake wa zamani katika maongezi yenu.
Leo kama Daktari Mapenzi tumeamua kukomesha hili janga kwa kuja na mbinu madhubuti ambazo zitamzingiti mwanaume kama huyu ili aweze kukufikiria wewe pekeake na wala si mwingine.
#1 Mpe muda.
Wakati mwingine ni bora zaidi kumpa mwenzako time ili aweze kusahau matukio ya awali. Mwanaume ambaye ameachana na mpenzi wake wa zamani kwa kawaida inaweza kuchukua muda mrefu kabla kurudi kawaida. So iwapo kweli unampenda mwanaume flani basi mpe muda anaouhitaji ili aweze kumsahau mpenzi wake wa zamani. Hilo si jambo baya kufanya.
Kumpa muda wa kufikiria kunasaidia kwa kuwa atakuwa anapoteza mawazo yake ya zamani na huyo mpenzi wake. Hakikisha unamkaa mbali kabisa ama anaweza kukuona kama nuksi ama kikwazo katika maisha yake.
#2 Kuwa rafiki yake na umpatie sapoti anayohitaji.
Jambo la kwanza la kufanya ni kuwa rafiki mzuri kwake. Ni kawaida kuwa na hisia za chini na mpweke wakati umetoka katika mahusiano. So ukiwa na tamaa ya kumrukia uanze mahusiano na yeye basi inaweza kukujeukia kwa sababu ishu zake bado hazijatatulika.
Kwa sasa unachohitajika ni kumwonyesha kuwa wewe ni rafiki yake mkubwa, msikilize kwa kila kitu atakachokuambia na pia umpatie sapoti anayoihitaji. Kufanya hivi kutamfanya akuone kuwa unamthamini na kukuona kama mtu aliyekuwa karibu yake muda huu ambao umekuwa wa majonzi kwake. Hata kama mambo uliyotarajia yafanyike kama vile ulivyokuwa unataka hayakufanyika, haitakuwa ni tatizo kubwa coz tayari ushaweka msingi mzuri wa yeye na wewe katika maisha yenu.
#3 Jiepushe asikuingize katika himaya ya urafiki.
Hapa ndipo kunakuja tatizo. Pindi utakapokuwa unaspend muda mwingi na yeye kwa kuenda kuangalia mpira pamoja, kutembea, kufanya shopping nk, tayari utakuwa ushaiteka atenshen yake. Lakini je, hii ndio atenshen umekuwa ukiitafuta?
Tatizo linakuja hapa: kuwa makini sana usijeuke kuwa kama “mmoja wa wanaume” ama unaweza kuwa mmoja wa wale –marafiki zake. Hakikisha unamake effort ya kuonekana mrembo, kuvutia, kuwa na confidence, na kufanya wale wanaume wengine wakunotice. Mfanye akuone wewe kama mchumba ‘mtarajiwa’ kwa kutangamana kama marafiki na pia uwe unampa ishara fioa/fiche za kumvutia.
#4 Hakikisha mnajuana.
Ijapokuwa hauwezi kumlazimisha aingie katika mahusiano na wewe, huu utakuwa wakati mzuri wa kujuana bila ya presha yeyote. Nendeni mkale bata pamoja kwa kufanya mambo ambayo nyote wawili mnapenda. Hakikisha unaifanya inakuwa ya furaha, ucheshi, na kumpa mazingara ambayo hayatukuwa na vituko wala drama zozote.
Kama tulivyotangulia kusema awali ni kuwa lazima uwe unatumia mbinu fioa kumwonyesha kuwa unapendezwa na yeye. Lakini usiwe na pupa la sivyo utamwogopesha.
#5 Kuwa makini na vichocheo.
Vichocheo vinaweza kuja kwa njia tofauti tofauti. inaweza kuwa marashi, sinema, nguo, mkahawa. Hivi vichocheo vinamkumbusha mpenzi wake wa zamani na jinsi walivyokuwa wakiinjoy maisha yao, jambo ambalo linaweza kuchubua vidonda vya moyoni ambavyo tayari amekuwa akijaribu kuviponesha.
So kuhakikisha kuwa hautaamsha hisia za mpenzi wake wa zamani basi lazima uepukane na vichocheo hivi. Kwa mfano iwapo alikuwa akienda katika mkahawa flani na mpenzi wake, basi huo mkahawa usithubutu kujaribu kupitia na hapo. Mavazi, marashi, vipodozi ambavyo mpenzi wake alikuwa akivitumia hakikisha kuwa unaviepuka kabisa. Hakikisha anasahau kabisa kuhusiana na mambo kama haya. Ukifanikiwa kutimiza jambo hili basi utakuwa wakati mzuri wa kwako kuanza kuifuta akili yake pole pole.
#6 Mwache aexperience uhuru wake.
Kuna mambo ambayo mwanaume huyu alikuwa akikosa wakati alipokuwa na mpenzi wake. So wewe haupaswi kabisa kuwa kizingiti kwake kujaribu mambo mapya. Hii inaweza kuwa kama vile kutembea na marafiki zake nyakati za usiku, kusafiri sehemu za mbali, ama kuspend wiki nzima nyumbani huku akicheza gemu zake. Mwache ajihisi huru. Mpe sapoti yote ambayo anahitaji. Pia umuelewe shida na matatizo yake.
#7 Jihusishe na activity za kimwili pamoja.
Aidha iwapo mnafanya mazoezi ama mapenzi, ni muhimu kuufanya mwili wake kuwa mchangamfu kila wakati ilimradi akili yake isijazwe na fikra za matukio ya awali. Kufanya mazoezi ya mwili kwa kawaida kunatoa misongo ya mawazo na kuleta hisia chanya kwa maisha.
Unaweza kumchangamsha kwa kufanya mapenzi ambayo hajawahi kuyapitia tangu kuzaliwa kwake ama unaweza tu kuamua kumshawishi aachane na tabia ya kufagia nyumba yake badala yake muende gym kufanya mazoezi pamoja. Na usisahau kumuonyesha maungo yake vile ambavyo inastahili.
#8 Ichangamshe confidence yake.
Mahusiano yake ya awali yanaweza kushusha kujiamini kwake. Anaweza kujiona hafai, na anaweza kuona kuwa hawezi kupata mwanamke mwingine mzuri kama mpenzi wake wa awali. Mjenge kwa kumsifia.
Anza na mambo madogo madogo kama vile kuongea kuhusu hairstyle yake mpya, tai yake, halafu uanze kuongea zaidi kuhusu jinsi anaweza kumudu muda wake vizuri ama jinsi anavyokuwa na uhusiano mzuri na wenzake. Mfanye ajione kuwa yeye ni bora zaidi kwa kumpatia atenshen inayohitajika. Hakikisha unampa atenshen nzuri ili aweze kuwa na fikra chanya maishani mwake.
#9 Mpe nafasi ya kufunga ukurasa.
Mara nyingi mtu anashindwa kuachana na mpenzi wake wa zamani kwa kuwa bado hajapata nafasi ya kufunga ukurasa. Kama hii ndio hali inayomkumba mwanaume ambaye unatoka naye, labda huu ndio utakuwa wakati mzuri wa kumpa nafasi afunge chapta kabisa na mpenzi wake wa zamani. Kama anahisi kuenda tu kuongea na yeye, mpatie uhuru. Inaweza kuwa tishio kwake na kwako, lakini labda hili ndilo jambo kuu ambalo anahitaji ili aweze kumuona mpenzi wake wa zamani kuwa mtu asiyekuwa na thamani yeyote maishani mwake.
Kumpa nafasi hii kunaweza kuwa mwisho wake wa kumfikiria mpenzi wake wa zamani kabisa.
#10 Kuwa wa thamani.
Unaweza kuwa umemsaidia muda huu wote aweze kumsahau ex wake na sasa fikra zake zote zimekuja kwako – lakini wewe umekuwa hapo tu kuuchezea wakati wake muda huu wote. Kama fikra zako ni kumchezea mwanaume huyu, tafadhali mpe nafasi aishi kivyake, usimtatize! Kufanya bidii kumsahau mtu halafu tena upitie janga lilo hilo ni jinamizi kubwa sana. Risk anayoichukua mara ya pili huwa inahitaji ujasiri wa hali ya juu, so hakikisha kuwa unakuwa thamani kwake kwa kuwa amejitolea kubahatisha kwako.
Upo!?
Habari...
ReplyDeleteSamahan na weza pata mawasiliano yako?